> #1:JE, UNAFAHAMU MFUMO WA ELIMU JUMUISHI?

#1:JE, UNAFAHAMU MFUMO WA ELIMU JUMUISHI?


SURA YA 1:

MALENGO:

KUJENGA JAMII YENYE USAWA NA FURSA KWA WOTE


MKUTASARI

Jiulize Maswali haya kabula ya kusoma

Je, elimu jumuishi ni nini? 

Kwa nini ni muhimu kuitekeleza?

 Ni faida zipi zinazotokana na mfumo huu wa elimu?

 Unakabiliwa na changamoto zipi? 

Taarifa hii inalenga kujibu maswali haya na kueleza umuhimu wa elimu jumuishi katika jamii.


Maana ya Elimu Jumuishi

Elimu jumuishi ni mfumo wa elimu unaohakikisha kuwa watoto wote, bila kujali tofauti zao kama ulemavu, jinsia, asili, au hali ya kiuchumi, wanapata fursa sawa ya kujifunza na kushiriki kikamilifu katika shughuli za shule na jamii.

Mfumo huu unaamini kila mtu ana haki ya kupata elimu bila kujali utofauti na changamoto aliyo nayo.

Makundi ya Watu Wanaohusika katika Elimu Jumuishi

Yapo makundi na aina mbalimbali za watu wanao paswa kupata haki hii na yanaweza kutokea katika hali mbalimbali kama changamoto zinazo onekana, zisizo onekana,na za kimazingira ambayo ni

  1. Wanafunzi wenye ulemavu unao onekana :nikundi linao tanbua walio na viashilia vinavyo onekana kwa macho  Mfano: Viungo kama mkono miguu,ulemavu wa Macho,Uziwi,Ulemavu wa ngozi(albinism)
  2. Wanafunzi wenye ulemavu usio onekana: nikundi linalo wataja wanafunzi wenye changamoto ili zibainike lazima wafanyiwe vipimo vya asili au kisasa mfanoUlemavu wa akili,Usonji
  3. Wanafunzi wenye changamoto za ujifunzaji: Awa ni wanafunzi wanao pata tabu katika kufanya shughuli za kielimu kama kusoma kuandika na kuesabu mfano wao ni Diskalukia,Afazia
  4. Wanafunzi wanao tokea katika mazingira magumu: kundi hili utokana na sababu mbalimbali kama malezi,balee,ajira za utotoni,vifo,Magonjwa Mfano Yatima ,Machokolaa
  5. Wanafunzi wanao tokea familia za kuamaama:zipo jamii ambazo adi waleo azikai sehemu moja asa za wafugaji na kuama kutafuta maji na Chakula na mtoto kukosa haki ya kielimu Mfano wa jamii izo ni Wamasai,Adizabe
  6. Wanao tokea familia za wakimbizi: kutokana na athari za vita uweza kuacha masomo na kukimbia mfumo huu uwapa nafasi ya kuludi darasani tena 




Umuhimu wa Elimu Jumuishi

Nimuhimu Elimu jumuishi kupewa nafasi kubwa katika jamii kutokana na faida zake kama ilivyo baadhi apo

  1. Kuhakikisha haki ya msingi ya elimu kwa kila mtoto.
  2. Kuondoa ubaguzi na unyanyapaa katika mazingira ya kujifunzia.
  3. Kukuza usawa na mshikamano katika jamii.
  4. Kuimarisha maendeleo ya kitaaluma na kijamii kwa wanafunzi wenye ulemavu
  5. Kwa wanafunzi wnye ulemavu: Kujifunza katika mazingira yenye msaada na kujengwa kujiamini.
  6. Kwa wanafunzi wasio na ulemavu: Kujifunza thamani ya tofauti na ushirikiano.
  7. Kwa jamii: Kujenga jamii yenye mshikamano na inayojali haki za kila mtu.
  8. Kiuchumi: Kusaidia watu wote kuwa na mchango katika jamii na uchumi wa taifa.



Changamoto Zinazokabili Elimu Jumuishi

Mfumo huu wa elimu umekuwa ukikumbwa changamoto mbalimbali na kusababisha kuwa ngumu kutekelezeka kama ifuatavyo

  1. Ukosefu wa miundombinu rafiki na vifaa saidizi.
  2. Ukosefu wa walimu wenye ujuzi wa kushughulikia mahitaji maalum.
  3. Uelewa mdogo wa jamii kuhusu umuhimu wa elimu jumuishi.
  4. Mtazamo hasi na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu.



Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Utekelezaji wa Elimu Jumuishi

  1. Mazingira ya kujifunzia yawe rafiki kwa wote (vifaa na miundombinu).
    Mfano wa darasa jumuishi

  2. Mafunzo maalum kwa walimu.
  3. Ushirikishwaji wa wazazi na jamii.
  4. Sera na miongozo inayoweka bayana haki za wanafunzi wote.
  5. Upatikanaji wa vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu.







Wadau na Wawezeshaji wa Elimu Jumuishi


1. Serikali

Kuunda na kutekeleza sera za elimu jumuishi.

Kutoa bajeti ya vifaa na miundombinu rafiki.

Kutoa mafunzo kwa walimu.


2. Walimu

Kutengeneza mazingira rafiki ya kujifunza kwa wote.

Kutumia mbinu za ufundishaji zinazojumuisha wanafunzi wote.

3. Wazazi na Walezi

Kushirikiana na walimu katika kusaidia watoto wao.

Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu jumuishi.

4. Taasisi za Kidini na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs)

Kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu haki za watu wenye ulemavu.

Kushirikiana na serikali katika uboreshaji wa miundombinu na vifaa saidizi.

5. Jamii

Kuondoa unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu.

Kutoa msaada wa kijamii na kisaikolojia kwa familia zenye watoto wenye ulemavu.


Mikakati ya Utekelezaji wa Elimu Jumuishi.

  1. Kuandaa sera madhubuti za elimu jumuishi zenye utekelezekaji.
  2. Kutoa mafunzo endelevu kwa walimu na watendaji wa elimu.
  3. Kuwekeza katika miundombinu na vifaa saidizi shuleni.
  4. Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutekeleza mipango ya elimu jumuishi.
  5. Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu jumuishi kupitia kampeni za uhamasishaji.


Elimu jumuishi ni msingi wa kujenga jamii yenye usawa, mshikamano, na maendeleo endelevu. Ni jukumu letu sote kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya kujifunza na kuchangia katika maendeleo ya jamii.

ITAENDELEA NA SEHEMU YA 2.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi