> IFAHAMU AFYA YA AKILI , SABABU NA MATIBABU.

IFAHAMU AFYA YA AKILI , SABABU NA MATIBABU.

 


Magonjwa ya Akili ni Nini?

Magonjwa ya akili ni matatizo ya

ubongo ambayo humfanya mtu

kuwa na hisia, fikira na matendo

tofautinayaleyanayotarajiwana

jamii na kushindwa kukabiliana

na changamoto za maisha.

husababishwa na Nini?

Magonjwa ya akili yanaweza

kusababishwa na sababu za

  1. kibaiologia au
  2.  kisaikolojia;

Sababu za kibiologia

• Kurithi vinasaba kutoka kwa

wazazi.

• Magonjwa ya muda mrefu kama

degedege, malaria kali, UKIMWI

nk

• Matumizi ya dawa za kulevya

Sababu za kisaikolojia

• Majanga, ubakaji, uvamizi, ajali,

utekaji nyara, kukosa elimu,

kukosa ajira nk

• Kufiwa, kutengana,talaka, ugoni,

kufungwa

• Kufukuzwakazi,kukosamishahara,

kustaafu kazi nk.

• Kutokufanya vizuri kwenye

masomo na Kufukuzwa chuo/

shule

• Matatizo yanayowaathiri watoto

kisaikolojia

 *  Kunyanyaswa kingono

 *  Kupigwa na kutengwa

 *  Kutothaminiwa

 *  Kutokupata matunzo stahiki

Dalili za Magonjwa ya Akili ni Zipi?

Magonjwa ya akili yapo ya aina

nyingi na dalili zake zinatofautiana

kati ya ugonjwa moja na mwingine.


Dalili za Kihisia

• Kusikia sauti ambazo watu

wengine hawazisikii

• Kuona vitu ambavyo watu

wengine hawavioni

• Kuhisi kufuatiliwa na watu

• Wivu uliopitiliza

• Kuhisi mawazo yake

yanajulikana na watu wengine

au yanazungumzwa kwenye

vyombo vya habari

• Kuhisi kuwa mtu anatumia

mawazo yake kufanya mambo

Fulani

• Kuhisi harufu ambayo watu

wengine hawaisikii

• Kuhisi maisha hayana thamani

na kuona bora kufa kuliko kuishi


Dalili za Kimwili

• Kukosa furaha au kuwa na furaha

kupita kiasi

• Kuwa na wasiwasi au woga

kupita kiasi

• Kupunguzakuongeaau kuongea

kupita kiasi

• Hasira za haraka na kufikia hatua

ya kudhuru watu au kuharibu

vitu.

• Kuwa na msongo wa mawazo

• Kujitenga na watu na kupenda

kukaa mwenyewe muda mwingi

• Kutokuwa na ari ya kufanya kazi

au kufanya kazi nyingi kwa wakati

mmoja bila ya kuzikamilisha

• Kutokuonyesha hisia yoyote usoni

mwake [furaha au huzuni]

• Kutokujijali usafi na muonekano

wake

• Mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili

una nguvu sana kupita kiasi

• Kukosa usingizi au kulala usingizi

sana kupita kiasi

• Kukosa hamu ya kula au kuwa na

hamu sana ya kula

• Kutokutulia (kuhamanika) au

kutulia sehemu moja muda mrefu

bila ya kujisogeza

• Maumivu sehemu mbalimbali

za mwili ambayo vipimo vya

hospitali havionyeshi tatizo lolote

la kimwili.


Dalili za Kiakili

• Kukosa umakini wa shughuli zake

za kila siku

• Kusahaukwaharakaaukupoteza

kumbukumbu

• Kukosa uwezo wa kupambanua

mambo kwa mitazamo tofauti

• Kutokujali

• Kuwa na imani zisizo za kawaida

kama vile;

Kuwa mtu maarufu au Nabii

*  Kupokea taarifa kutoka

kwenye redio au mitandao

ya simu

*  Imani ya kuwasiliana na watu

maarufu

*  Kuamini kuwa na nguvu ya

ziada kutoka nje ya mwili

*Imani kuwa kuna watu

wanamfuatilia/ wanataka

kumdhuru

• Mawazo yake hayana mtiririko

unaoeleweka.

Matibabu ya Magonjwa ya Akili

Matibabu ya magonjwa ya akili

hutoafautiana kati ya ugonjwa

mmoja na mwingine

  1.   Elimu kwa jamii kuhusiana na

magonjwa ya akili ni kitu cha

muhibu sana katika kuzuia

kujirudia au kupata ugonjwa wa

akili, juu ya matibabu na msaada

anaohitaji mgonjwa ili kuendelea

na maisha yake ya kila siku.  

2.Kupatiwa uchunguzi mapema

ili apatiwe tiba sahihi na ya

mapema

3.  Tiba ya kisaikolojia (kujitambua

aliko, anapotaka kuwa na

kuamua kufanya mabadiliko

kwa kutegemea uwezo wake

mwenyewe

4. Tiba kimwili kutumia dawa za

hospitali

5. Matibabu kwenye nyumba za

upataji nafuu (Sober Houses)

6.  Ushirikiano kati ya mgonjwa

familia na wataalamu wa tiba

huleta mafanikio makubwa sana

katika matibabu.

7.  Kutokutumiamadawayakulevya

ikiwa ni pamoja na vilevi

8. Pata muda mrefu wa kupumzika

9.  Fanya mazoezi

10.  Usijitenge na jamii

11.  Kujibidisha kwenye shughuli za

kuleta kipato

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi