> MPIRA WA KENGELE (GOAL BALL)

MPIRA WA KENGELE (GOAL BALL)

 



Mpira wa kengele au ‘Goal ball’ ni mchezo

HISTORIA

ulioanzishwa na raia wa Australia, Hanzi Lorenzen na raia wa Ujerumani, Sepp Reindle mwaka 1946 kwa ajili ya kuwasaidia askari waliopigana vita ya pili ya dunia na kupata matatizo ya macho.Na kuwa mchezo maarufu unao chezwa na watu wenye ulemavu wa uoni Mfano katika mashindano makubwa ya Par Olympic

MCHEZO

Washiliki

huchezwa na washiriki watatu wasioona, au wenye uono hafifu ambao hufungwa vitambaa usoni, ambapo mchezaji atalazimika kuucheza kwa kutumia hisia za kengele kwani mpira wenyewe unapoburuzika ni rahisi kuusikia mlio wa kengele hivyo na utazuiwa kwa kuudaka.

MUDA.

unaochezwa kwa dakika 24, dakika 12 kila upande na dakika 5 za mapumziko

UWANJA.

goli linalotumika kwa kila upande lina upana wa mita 9 wakati uwanja mzima una ukubwa wa mita 18 sawa na uwanja unaotumika kwa ajili ya mpira wa wavu (volleyball).

VIFAA

Vipo vifaa mbalimbali kwa ajili ya mchezo huu miongoni ni

  1. Mpira wa kengele
  2. Firimbi
  3. Kitambaa/viraka vya jicho/Miwani
  4. Sale
  5. Zuria
  6. Koni

UNAVYO CHEZWA
Mchezo huu huchezwa na washiriki watatu wasioona, au wenye uono hafifu ambao hufungwa vitambaa usoni, ambapo mchezaji atalazimika kuucheza kwa kutumia hisia za kengele kwani mpira wenyewe unapoburuzika ni rahisi kuusikia mlio wa kengele hivyo na utazuia kwa kuudaka.

Amesema goli likiingia refa atapuliza filimbi mara mbili, na endapo mchezaji atarusha kuelekea upande wa pili ukiwa juu bila kuburuzika, refa atapuliza filimbi kutoa adhabu ya penati ambapo refa atawatoa wachezaji wawili na kumbakisha mmoja ili aweze kudaka penati.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi