> MICHEZO INAYO CHEZWA NA WATU WENYE ULEMAVU

MICHEZO INAYO CHEZWA NA WATU WENYE ULEMAVU

 


Ipo michezo mbalimbali inayo weza kuchezwa na Mtu, Watu au lika la watu tofauti tofauti kwa malengo yale yale ya michezo ikiwemo

  • Kuburudisha
  • Kupunguza na kuondoa msongo wa mawazo
  • Kuelimisha 
  • Kuibua vipaji
  • Na ajira
Kwa kuzingatia umuhimu uo ivyo na watu wenye ulemavu na wao wana michezo mbalimbali iliyo fanyiwa marekebisho na maboresho kwa malengo ya kuwapa haki izo kama watu wengine na ili iweze kuwa rafiki lazima ifanyiwe Urekebifu mbalimbali kwa kuzingatia miongoni mwa vipengele vifuatavyo
  1. Urekebifu wa Muda
  2. Vifaa
  3. Uwanja
  4. Sheria na kanuni za mchezo
ANGALIZO

Mtu mwenye ulemavu wa aina yoyote anapo shiliki, kujifunza Michezo ni muimu kuzingatia mambo muhimu kama . 

  1. Muda
  2. Usalama
  3. Aina ya ulemavu
  4. Upatikanaji wa Taarifa sahii na miongozo
  5. Matumizi sahii ya vifaa vya michezo





IFUATAYO NI MICHEZO ILIYO FANYIWA UREKEBIFU NA WANAWEZA SHIRIKI.


1. GOAL BALL 

Ni mchezo maalum kwa watu wenye ulemavu wa kuona.

Mipira ina kengele ndani yake, na wachezaji hutegemea sauti ya mpira kuutambua.

Unachezwa kwa kurusha mpira kuelekea goli la mpinzani huku ukitumia ulinzi wa mwili kuuzuia.




2. KUKIMBIA KWA KUTUMIA KITI CHA MAGURUDUMU (Wheelchair Racing)

Wanafunzi wanaotumia viti vya magurudumu wanashiriki mashindano ya kukimbia.

Viti vya magurudumu vya kimbiaji hutengenezwa maalum kwa kasi na wepesi.


3. BASKETBALL YA VITI VYA MAGURUDUMU (Wheelchair Basketball)

Mchezo wa mpira wa vikapu unaochezwa na wachezaji walioko kwenye viti vya magurudumu.

Sheria zake ni sawa na za kawaida, lakini zimebadilishwa kidogo kukidhi mahitaji ya wachezaji.


4. BOCCIA

Mchezo wa kurusha mipira kwa usahihi, unaofaa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa viungo.

Wachezaji hutumia mikono, miguu, au vifaa maalum kurusha mipira.


5. SOKA YA WATU WENYE ULEMAVU WA MIGUU 


Wachezaji hutumia mikongojo kucheza mpira, huku sheria zikiwa zimebadilishwa.

Inahusisha wachezaji wenye mguu mmoja au walio na ulemavu wa miguu.


6. RIADHA ZA WATU WENYE ULEMAVU (Paralympic Athletics)

Wanafunzi hushiriki katika mbio, kurusha mkuki, tufe, au kuruka, kulingana na uwezo wao.

Vifaa na viwanja vinabadilishwa ili kufanikisha ushiriki wao.


7. KUOGELEA (Adaptive Swimming)

Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo au kuona hushiriki katika mashindano ya kuogelea.

Mbinu za uogeleaji na vifaa kama maboya hubadilishwa.


8. Sitting Volleyball

Ni mchezo wa mpira wa wavu unaochezwa wakiwa wamekaa chini.

Unafaa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa miguu au viuno.


9. Mbio za Baiskeli (Hand Cycling)

Hutumia baiskeli maalum inayosukumwa kwa mikono badala ya miguu.

Hufaa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa miguu.


10. Chess na Michezo ya Akili

Hii ni michezo inayojumuisha soka ya akili kama vile chess, scrabble, au michezo mingine ya kimkakati.

Inafaa kwa wanafunzi wenye changamoto za viungo au mawasiliano.


Michezo hii inatoa nafasi ya ushirikiano na maendeleo kwa wanafunzi wenye ulemavu, hivyo ni muhimu kuweka mazingira yanayojumuisha wote.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi