> VITA YA MAJI MAJI 1905-1907

VITA YA MAJI MAJI 1905-1907

 


Vita ya Maji Maji ulikuwa upingaji mkali wa Makabira ya   kusini mwa Tanganyika dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ujerumani katika maeneo ya kusini ya koloni la Afrika Mashariki ya Kijerumani.

Vita hivyo vilishirikisha baadhi ya makabila ya kusini mwa Tanzania ya leo dhidi ya sera ya Kijerumani iliyoundwa kwa nguvu kuwalazimisha watu wa Tanganyika kulima zao la pamba.

Vita hivyo vilidumu kuanzia mwaka 1905 hadi 1907.

wakoloni waliwataka wanajamii kulima mazao ya kibiashara na walikatazwa kulima mazao ya chakula; kwa mantiki hiyo wanajamii walilima mazao ya biashara na kuacha kulima mazao ya chakula kwa lengo la kuwanufaisha wakoloni huku wao wakipata njaa kwa sababu ya kutolima mazao ya chakula kwa ajili ya kuwapatia chakula na huku adhabu kali ikitolewa kwa wale watakaopinga.

Kwa sababu hiyo wananchi walilazimika kufanya kazi huku wakilipwa mshahara mdogo au kutolipwa kabisa. Watu ambao hawakulazimika kufanya kazi ni watoto wadogo na wazee; kwa wale vijana wenye nguvu walifanyishwa kazi ngumu lakini kwa upande wa wasichana na mama wajawazito waliufanya kazi za ndani.

Hivyo basi waliamua kukataa manyanyaso na masumbuko dhidi ya wakoloni.

Mtemi wa kabila la Wangindo Kinjekitile Ngwale Aliamua kupigana na wakoloni na aliamini kwamba maji ndiyo silaha ya kipekee ambayo ingetumika kuwashinda wakoloni hata akawaambia wananchi wake kwamba wakoloni wakirusha silaha waseme "maji" kwa madai ya kuwa silaha itabadilika na kuwa maji.

Wanajamii wake waliamini kusikiliza, kwa hiyo basi vita ilipoanza wakoloni walipoanza kuwashambulia wanajamii walisema, "maji", lakini jinsi walivyokuwa wakisema "maji" ndivyo walivyozidi kushambuliwa.

madhara makubwa waliyoyapata: ni wanajamii wengi walipoteza maisha kwa hiyo nguvukazi ilipungua kwa kiwango kikubwa, lakini  chanzo kikubwa kabisa ni kupinga manyanyaso.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi